Sunday, 12 January 2014

ukorofi

eti ni haki upatapo utakacho
hata cha mwenzio hujui kufumbia macho
rafiki ndiye adui, yaani yeye ndiye kikulacho

watabasamu tuwapo pamoja sana
ila niondokapo unanisema sema
laiti ungejua nilivyokufariji wangu msena
mdomo ungeufunga usije kuniongea tena

kwa hakika mimi pia nina yangu makosa
la kwanza kwenye orodha, dadako kumposa
hiyo ndoa yaonekana taabani kanitosa
kwani tokea hapo, uliniona adui asilimia tisa tisa

ni nadra kumpata mwendani akufaaye kwa ndani
lakini mimi, kabla ya lawama, jua dadako namdhamini
hukutaka tuwe pamoja, lakini mapenzi ni kipofu, wewe kaniambia hivyo mimi

wewe pia una ndoa yako ulipo
basi iwache yangu istadi, usiivamie kipopo
kwangu napenda, tatizo likiibuka, nagonga ndipo!
ili upate kujua, wakati gani unikerapo !
popo wewe!
©  2013


No comments:

Post a Comment

comment

Highlights

When you smile,  I pray that it's because of me When you cry,  I pray that only I can wipe the tears away When you are happy I pray th...